728x90 AdSpace


Hivi Punde

Saturday, June 18, 2016

HABARI: BAADA YA CHIDY SASA NI RAY C, SOBER HOUSE


Siku chache baada ya kusambaa kwa video ikimwonyesha Rehema Chalamila maarufu kama Ray C akichukuliwa na gari ya polisi, kwenye mitandao ya kijamii iliandikwa Ray C alitaka kujiua, japo ukweli ni kwamba inaonekana bado anasumbuliwa na madawa. Pia ilisadikika kwamba alikamatwa na kupelekwa polisi, si kweli, Polisi walimchukua na kumpeleka hospitali kwa ajili ya msaada kwa mwana dada huyo ambaye alionekana kuwa na hali mbaya jioni ile na angeweza kupoteza maisha.

Pamoja na juhudi kubwa ya mheshimiwa raisi mstaafu wa awamu ya nne Dr. Jakaya M. Kikwete na Bw. Ruge Mutahaba wa Clouds Media Group kumsaidia msanii huyo wa bongo fleva, rnb na taarabu 'Ray C' bado hali imekuwa tete baada ya kurudia tena madawa mda mfupi baada ya kuonesha mafanikio makubwa ya kupona.

Siku moja kabla ya tukio ilifanyika mipango ya kumpeleka Ray C kwenye nyumba ya matibabu ya watu walioathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya 'SOBER HOUSE' huko bagamoyo alikotoka Chidy ambaye kwa sasa anaendele vizuri. Ambako ameshapelekwa tayari kwa hiari yake pasipo kulazimishwa.

"TUMUOMBEE RAY C MAANA HAKUPENDA KUWA VILE NA HAKUNA AIJUAYE KESHO YAKE!"


"DAAH!!! HAYA MADAWA NI NANI ANAYAINGIZA??? ONA WASANII WAZURI WANAVYOPOTEZWA NA MADAWA HAYO YA KULEVYA! SERIKALI YETU ITUSAIDIE VIJANA TUNAANGAMIZWA NA MADAWA"

.................Eddy Entertainment inamtakia kila la kheri Ray C.........
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: HABARI: BAADA YA CHIDY SASA NI RAY C, SOBER HOUSE Description: Rating: 5 Reviewed By: Eddy
Scroll to Top