Ilikuwa ni tuzo ya msanii bora kutoka Afrika, ambapo katika kategori hiyo ilikuwa na wasanii wafuatao:
1.WIZKID (NIGERIA)
2. AKA (SOUTH AFRICA)
3. SERGE BEYNAUD (COTE D’IVOIRE)
4. CASSPER NYOVEST (SOUTH AFRICA)
5. MZVEE (GHANA)
6. YEMI ALADE (NIGERIA)
7. DIAMOND PLATNUMZ (TANZANIA)
8. BLACK COFFEE (SOUTH AFRICA)......MSHINDI
Jina lake halisi ni Nkosinathi Innocent Maphumulo, jina lake la kisanaa/kimuziki anaitwa Black Coffee/ Dj Black Coffee, alizaliwa tar. 11March 1976 (miaka 40) huko Durban, Afrika kusini.
Black Coffee ni muandaaji wa muziki (record producer), DJ, mwimbaji/msanii pia mjasiriamali. Alianza kuonekana sana kwenye tasnia ya muziki mnamo mwaka 1995 na anafanya vizuri mpaka leo.
Mwaka 2011, Black alifanikiwa kufunga ndoa na muigizaji na mwongozaji wa filamu Bi. Mbali Mlotshwa, familia ya Coffee imebahatika kuwa na watoto wanne, ambapo wawili ni watoto wa mke wake wa sasa (Mbali Mlotshwa) na wawili ni wa mahusiano yaliyopita ya star huyo (Black).
Mpaka sasa Coffee ametoa albamu 5 ambazo ni Black Coffee (2005), Have Another One (2007), Home brewed (2009), Africa Rising (2012) na Pieces of Me (2015).
Zifuatazo ni tuzo ambazo Black Coffee amewahi kupata.
2005: | SAMA Best Urban Dance Album |
2010: | South African Music Awards#12th South African Music Awards .282006.29 |
2010: | SAMA Best Male Artist |
2010: | Health Magazine Best Man |
2010: | Metro FM Award for Best Produced Album |
2010: | Metro FM Award for Best Dance Album |
2011: | Channel O Award for Most Talented Male Artist |
2012: | Sunday Times Generation NEXT Award for Coolest DJ |
2013: | SAMA Best Dance Album |
2013: | Sunday Times Generation NEXT Award For Coolest DJ 2013 |
2014: | Sunday Times Generation Next Award for Coolest DJ |
2015: | DJ Awards for Breakthrough DJ Of The Year |
2016: | SAMA Best Dance Album |
BET Award for Best International Act: Africa |
Tunaamini katika kila shindano kama hili lazima apatikane mshindi mmoja na haimaanishi walioshindwa hawajui au hawafai, ni wakali ila inatakiwa apatikane mkali mmoja hivyo Hongera sana kwa wote waliokuwa 'Nominated' kwenye kategori hiyo. Hongera sana kwa Diamond platnumz kwa kuwa mmoja wapo na kuiwakilisha Tanzania katika tuzo hizo. Hongera nyingi kwa Black Coffee kuwa mshindi katika kategori hiyo na kuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika Kusini kupata tuzo ya BET. |
0 comments:
Post a Comment